Tanzania yaanza vema harakati za kuwania kufudhu kucheza mashindano ya U20 ya dunia
Timu ya Taifa ya wanawake U20 imeanza vema harakati za kuwania kufudhu kushiriki michuano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kufanyika Novemba, 2020 huko Panama na Costarica baada ya kuwachapanga Uganda kwa jumla ya mabo mawili kwa moja, na kuwaduwaza Waganda.
Mabao yaliyofungwa na Diana Lucas Msemwa mwenye jezi namba sita na ‘Opa Clement Tukumbuke’ aliyetinga jezi namba saba yalifanya wachezaji wa kikosi cha U20 cha Taifa, mashabiki pamoja na Watanzania kutoka uwanjani wakiwa na furaha kubwa na matumaini ya kufudhu kushiriki michuano hiyo mikubwa kabisa duniani.
Katika mchezo huo ni Uganda ndio walikuwa wakwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza, bao lililodumu kwa kipindi chote; mpaka timu zinakwenda mapumziko Uganda walikuwa wakiongoza kwa bao hilo lililofungwa na mshambuliaji machachali mwenye jezi namba tisa anayeitwa Nalukenge Juliet baada ya kuunguunganisha krosi kwa kichwa.
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya U20, Bakari Shime amesema kuwa ushindi huo ilikuwa ni matarajio yake yeye pamoja na benchi lake la ufundi, na kwamba walichokifanya Wanganda ni kuwawahi tu kwani yeye alijua kabisa kwamba Uganda wasingelishambulia kwa kuwa walikuwa ugenini hali ambayo ilikuwa tofauti kiuhalisia katika pichi.
Aidha kocha alibainisha kuwa kikosi cha Uganda sio kibaya ni kizuri sana lakini baada ya Waganda hao kupata bao la kwanza ilimlazimu kocha Shime kubadili mfumo wake alioanza nao kipindi cha kwanza jambo ambalo anaamini ndilo lililompatia matokeo hayo.
Kwa upande wa kocha wa Uganda Mbekeka Oliver, yeye anasema kuwa wachezaji wake walishindwa kuzingatia kilichotakiwa kufanywa hasa baada ya kuongoza wakabweteka na kujua kuwa tayari wameimaliza kazi, ndio maana wakapunguza kasi na ndipo Tanzania nao wakatumia nafasi hiyo kuwashambulia na hatimaye kuweza kurejesha goli na kisha kuongeza goli la pili lililowafanya washinde mechi hiyo.
Hata hivyo kocha Oliver alisema kuwa atajipanga vema katika mchezo wa marudiano utakao pigwa nchini Uganda siku chache zijazo.
Mchezo kati ya Tanzania na Uganda ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili; huku historiaya hivi karibuni ikiwabeba zaidi Watanzania kwa kushinda licha ugumu ambao hujitokeza kila timu hizi mbili zinapokutana.
Kikosi cha Tanzania kilichoanza ni; Aisha Ismail (GK JN.21), Protasia Mbunda (JN.3), Janeth Mambanza(JN.5), Enekia Kasonga(C, JN.17), Christopher Esther(JN.8), Diana Lucas Msewa (JN.6), Opa Clement Tumbukane (JN.7), Irene Elias Kisisa JN. 19), Pheromena Daniel (JN. 9), Aisha Masaka(JN. 10) na Julietha Singano (JN.16). Wachezaji walioanzia benchi ni; Tausi Abdallah (GKJN. 1), Eva Wailes(JN.2), Violeth Thadeo(JN.11), Shamim Ally (JN.12), Anastazia Nyandago(JN.13), Elimiana Mdimu(JN. 15) na Joyce Meshaki (JN. 20).