Tanzanite Yarejea Nyumbani
Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” imewasili nchini Machi 18, 2024 ikitokea kwenye mashindano ya All African Games yaliyokuwa yakifanyika Accra nchini Ghana.
Tanzanite iliyoondoka hapa nchini tangu Machi 9, 2024 ilicheza mechi tatu ikiwa nchini humo huku ikiwa haijafanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ambapo katika mechi zake ilizo cheza hatua ya makundi. Timu hiyo ilifanikiwa kutoka sare michezo miwili kwenye kundi A lililojumuisha timu nyingine tatu; Ethiopia, Ghana na Uganda.
Mchezo wa kwanza Tanzanite ilimaliza kwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya timu ya Uganda, mchezo wa pili ikipoteza kwa magoli 2-1 dhidi timu mwenyeji “Ghana” na ikamaliza hesabu zake kwa hatua hiyo Kwa matokeo ya sare nyingine ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ethiopia kwenye mchezo wa mwisho.
Hata hivyo, matokeo ya jumla ya Tanzanite hayakuweza kuiruhusu timu hiyo kusonga mbele zaidi kutokana na tofauti ya alama na timu nyingine za kundi hilo na uhitaji wa timu zinazotakiwa kusonga mbele kufuatia kanuni za mashindano hayo.
Tanzanite ilivuna alama mbili timu kwenye mechi zake tatu, huku ikimaliza kwenye nafasi ya tatu kwenye kundi, ikifuatiwa na Ethiopia ambayo ilimaliza mkiani ikiwa imebeba alama moja pekee.
Kwenye kundi hilo ni timu ya Taifa ya Ghana na Uganda ndizo zilizofanikiwa kusonga mbele baada ya kumaliza kwenye nafasi mbili za juu. Sasa Tanzanite itakuwa inajiandaa na kujiweka sawa na mashindano mengine, ambapo ni pamoja na nyota wa timu hiyo kuungana na timu za vilabu vyao kwaajili ya kuendelea na mechi za ligi zinazotarajia kuendelea kwa mzunguko wa pili.