Tanzanite Yashindwa Kutamba kwa Uganda
Timu ya Taifa ya Tanzania Tanzanite inayoshiriki mashindano ya CECAFA Women’s U20 Championship 2021 kwa mara nyingine imepoteza kwenye mchezo wake wanne dhidi ya Uganda baada ya kufanya hivyo pia kwenye mchezo wake uliopita dhidi ya Ethiopia.
Mchezo huo waliocheza dhidi ya Uganda Novemba 06, 2021 majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Njeru nchini Uganda umemalizika kwa timu ya Tanzanite kukubali kipigo cha bao 1-0, bao lilipatikana kwa mkwaju wa penati mnamo dakika ya 73 ya mchezo huo.
Licha ya mchezo huo kuonekana mgumu kwa timu zote mbili ambapo kwa Tanzanite ilionekana kutaka walau ushindi ili kujiweka pahala pazuri kwenye mashindano hayo baada ya kuwa tayari ilishapoteza alama nyingine tatu muhimu kwenye mchezo uliopita uliopigwa kwenye uwanja huo Novemba 03, 2021 bado iliwawia vigumu kujinasua kwenye mbinu za Uganda ambao wameonekana kuwa mbogo kwenye mashindano hayo.
Kwasasa timu zote sita shiriki kwenye mashindano hayo zimesaliwa na mchezo mmoja wa kukamilisha raundi ya tano nay a mwisho kwenye mashindano hayo ambapo mpaka kumalizika michezo hiyo yote ya raundi ya nne iliyopigwa hii leo bado anaonekana Uganda kusalia kileleni akiongoza kwa alama nyingi zaidi.
Matokeo ya mechi nyingine za leo ni; Eritrea 2-0 Djibouti na Burundi 0-1 Ethiopia; kwa matokeo hayo Tanzanite inaonekana kumaliza mashindano ikiwa nafasi ya tatu ambapo mchezo wao wa mwisho inatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Djibouti.
Kikosi kilichoanza dhidi ya Uganda; Husna Zuberi (JZ 18),Noela Patrick (JZ 02), Mwanamvua Haruna (JZ 16), Emiliana Isaya (JZ 15), Christer Bahera (JZ 17), Shehat Juma (JZ08), Rehema Ramadhani (JZ 14), Aisha Masaka (JZ 10) na Aisha Juma (JZ 09).
Kikosi cha akiba; Violeth Nicholaus, Esther Mabanza, Protasia Mbunda, Kadosho Shekigenda, Joyce Leman a Mariam Yusuph.