Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

TBC na TFF Waingia Mkataba Matangazo ya Redio

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  rasmi Agosti 3, 2021 imeingia mkataba wa miaka 10 na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)  wa haki za kurusha matangazo  yanayo beba maudhui ya mechi za Ligi Kuu Soka Bara kuanzia msimu wa 2021/2022.

Hafla hiyo fupi ya kusaini mkataba  huo wenye thamani ya fedha za Kitanzania shilingi Bilioni 3 limesimamiwa kwa ukaribu na Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF  ndugu Boniface Wambura na kuhudhuriwa na viongozi mbalibali kutoka TFF na TBC pamoja na vyombo vya habari vingine .

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC Gabriel Ndeomaki alisema kuwa TBC ni chombo chenye mtandao mpana zaidi katika kurusha matangazo nchini kulinganisha na vyombo vingine vya habari hivyo ni rahisi kufikia idadi kubwa ya watanzania kila mahali nchini na nje ya mipaka ya nchi.

Aidha aliongeza kuwa TBC kama chombo cha UMMA inadhima ya kuhamasisha hari na burudani katika mashindano mbalimbali nchini hususani kuitangaza Nchi kupitia mchezo wa soka, mchezo ambao umezidi kushika kasi kwa ligi kuu kupitia msimu ulioisha 2020/2021 kushika nafasi ya nane Afrika.

Kwa upande wa Rais wa TFF Wallece Karia alisema kuwa ni hatua kubwa kwa TFF kuingia mkataba wa aina hiyo ambao haukuwahitokea kwa Shirikisho kwa kipindi chochote  na kwamba wao wapo tayari kupokea mkataba wowote ule ilihali ni katika kuhakikisha wanazidi kukuza soka nchini. Rais Karia amewahakikishia kuwa maslahi yao yatalindwa na kwamba hakuna chombo kitakachoruhusiwa kurusha matangazo hayo kupitia redio pasipo kuwasiliana na TBC na TFF wala  kufuata taaratibu za kimkataba.

Rais Karia alieleza kuwa pesa hiyo itakayopatikana kupitia mkataba huo watakwenda kuigawa sawasawa kwa vilabu vyote vitakavyoshiriki Ligi Kuu kuanzia msimu ujao; tofauti kidogo na pesa za haki za matangazo kwa njia ya Televisheni ambazo zenyewe zitagawiwa kulingana na nafasi ya klabu kwenye msimamo wa ligi (kula kwa nguvu yako).

Rais Karia alibainisha akisema kuwa moja ya vipaumbele vyake  wakati akiomba ridhaa ya kuongoza TFF ilikuwa na kuimarisha maeneo ya masoko ili kuhakikisha wanaongeza wadhamini pamoja na kuhakikisha kuwa kila fedha inayopatikana kwa njia ya mpira wa miguu kutumika kwenye huo Mpira pia.

Viongozi waliohudhuria kwa upande wa TFF ni; Rais wa TFF Wallece Karia, Katibu Mkuu Kidao Wilfred pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ya TFF,  wakiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Mashindano TFF Salum Madadi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo na viongozi wengine.

Kwa upande wa viongozi wa TBC; alikuwepo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Gabriel Ndeomaki, Mkurugenzi wa huduma za Redio Aisha Datch, Mkurugenzi wa masoko Dafloza Kimboli na Mwanasheria wa TBC Msomi Gwakisa.

Mkataba huo hauwafungi wadau wengine wa vyombo vya Habari kurusha matangazo ya ligi kuu isipokuwa kwa makubaliano rasmi kati yao na TBC na TFF.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.