Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepata taarifa za Tukio la rushwa ya upangaji matokeo katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza(FDL) kati ya Rhino Rangers ya Tabora na Dodoma FC ya Dodoma.
TFF inaendelea kufuatilia kwa karibu,itawasiliana na Mamlaka zinazofanya kazi ya uchunguzi nchini kubaini ukweli wa jambo hilo.
Itakapobainika kulikuwa na nia ya kupanga matokeo hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika kwa mujibu wa taratibu.
Wakati huu ambapo TFF inafuatilia inawaomba wapenzi wa Mpira wa Miguu kuliacha suala hili kwa Mamlaka husika.