Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na benki ya KCB.

Mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 495,600,000 + VAT, umesainiwa leo mchana baada ya pande mbili kukubaliana.

Udhamini huu unaongezeka shilingi Milioni 75,000,000 (Milioni Sabini na Tano) baada ya ule wa awali kuwa Milioni 420,000,000 (Milioni Mia Nne Ishirini).

KCB Bank wamekuwa waumini wazuri katika kuendeleza soka la Tanzania baada ya kudhamini Ligi hii kwa miaka mitatu mfululizo.

Udhamini wa kwanza ulikuwa Milioni 325,000,000 (Mia Tatu Ishirini na Tano)msimu wa 2017/2018, 420,000,000 (Milioni Mia Nne Ishirini) msimu wa 2018/2019 na 2019/2020 Milioni 495,600,000