TFF yaendesha mafunzo ya soka la ufukweni kwa wanawake

Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia idara ya ufundi limeendesha mafunzo ya kwanza ya soka la ufukweni kwa wanawake yaliyofanyika Makao Makuu ya TFF, Ilala, Dar es salaam.

Mafunzo hayo ya siku mbili chini ya kocha Boniface Pawasa yamelenga kutoa elimu ya awali kwa wanawake kuhusu soka la ufukweni na namna ambavyo linachezwa ili kuleta ushindani katika mchezo huo ambao umezoeleka kuchezwa na wanaume.

Akizungumza baada ya kuhitimisha mafunzo Pawasa alisema, huu ni mpango mkakati wa kuendeleza soka la ufukweni na kuutambulisha rasmi kwa wanawake.

“Tff imejipanga kuhakikisha soka la ufukweni linafanya vizuri kwa pande zote wanaume na wanawake ndio maana ilianzaa kutoa semina kwa makocha wa vilabu mbalimbali vya wanawake ili wawe na uelewa wa namna ya kufundisha mchezo huu, nina imani wanawake watafanya vizuri zaidi katika soka la ufukweni” alisema Pawasa.

Timu zilizoshiriki ni Sayari Women, Ilala Queens, JMK Queens na Masala Princess.