Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leo Jumanne Machi 5,2019 limeendesha Semina ya siku moja ya Makatibu wa Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa iliyofanyika kwenye Hoteli ya DEMAGE,Kinondoni.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema TFF inaendelea na juhudi kubwa ya kuwajengea uwezo viongozi wanaofanya kazi na TFF.

Semina hizi ni muhimu katika maendeleo ya Mpira wa Miguu hapa nchini zikisaidia kuwa na lengo moja la maendeleo ya Mpira wa Miguu

Kwa Mwaka huu 2019 mbali ya kuwekeza kwenye maendeleo ya soka la Vijana juhudi kubwa ya TFF ni kuwajengea uwezo watendaji na viongozi.

Tayari TFF imefanya semina mbalimbali za kujenga uwezo zikiwemo semina ya Viongozi wa Ligi Kuu ya Wanawake,semina ya Waamuzi wa Kike na leo imefanyika semina ya Makatibu wa Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa.

Bado TFF itaendelea kufanya semina nyingine nyingi zikiwemo za Viongozi wa klabu za Ligi mbalimbali,Waamuzi,Makocha na Waandishi wa Habari.

Makatibu wa Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa wametakiwa kuzingatia yale ambayo wameyapata kupitia semina hiyo kwa faida ya maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania.

Makatibu kutoka Mikoa yote ya Tanzania wamehudhuria katika semina hiyo