Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewaondoa kwenye orodha ya Waamuzi wa msimu huu Waamuzi Abdallah Kambuzi,Godfrey Msakila na Consolata Lazaro.
Waamuzi hao waliochezesha mchezo kati ya KMC na Simba uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba Aprili 25,2019 wanaondolewa kwenye orodha ya Waamuzi wanaochezesha msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL) baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha kwenye mchezo huo.
Katika mchezo huo Kambuzi alikua Muamuzi wa kati kati akisaidiwa na Muamuzi msaidizi namba 1 Godfrey Msakila na Muamuzi msaidizi namba 2 Consolata Lazaro.
TFF inawaonya Waamuzi kuwa makini katika uchezeshaji wao na inafuatilia kwa karibu mienendo ya Waamuzi wote wanaochezesha Ligi Kuu,Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili,yeyote atakayebainika kuchezesha chini ya kiwango kwa namna yoyote atachukuliwa hatua stahiki.