Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaonya wote wanaotumia vibaya nembo ya TFF kutangaza gharama za hoteli na kusafirisha Watanzania kwenda Misri kwenye AFCON.

TFF inawataka kuacha mara moja kusambaza taarifa au vipeperushi vyenye nembo ya Shirikisho ambayo ni matumizi mabaya ya nembo ya Taasisi.

Yeyote atakayeendelea kusambaza vipeperushi hivyo kwa kutumia nembo ya TFF atachukuliwa hatua kali za kisheria.

TFF haijawahi kukubaliana na Taasisi yoyote wala kutangaza kuhusu gharama ya nauli na hoteli kwa wanaotaka kwenda Misri kwenye AFCON.

Kwasasa Shirikisho lipo katika hatua za mwisho kutangaza utaratibu ambao utatumika kwa mashabiki ambao wanataka kwenda nchini Misri katika fainali hizo.

Ieleweke kua TFF ina utaratibu wake wa namna ya kutoa taarifa zake mbalimbali.