Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kampuni ya Romario Sports 2010 LTD wamesaini Mkataba wa miaka mitatu kuzivalisha Timu zote za Taifa.

Kampuni ya Romario itakuwa inazivalisha Timu zote za Taifa kwa kipindi chote cha Mkataba huo.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema mbali ya Romario kuzivalisha timu za Taifa pia itatengeneza vifaa mbalimbali vya Michezo ikiwemo mipira.

Amesema TFF itafaidia kwa kupata sehemu ya asilimia katika mauzo ya vifaa vyote vyenye nembo ya TFF vitakavyoingizwa na Kampuni hiyo.

Ameongeza kuwa kabla ya kufikia makubaliano na Romario TFF ilifanya utafiti wa Makampuni mbalimbali yanayotengeneza vifaa vya michezo.

Aidha Rais Karia amesema kitendo kilichofanyika kusaini Mkataba huo ni chenye manufaa makubwa kwenye Mpira wa Tanzania.