Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom wamesaini Mkataba wa miaka 3 wa Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mkataba huo unathamani ya shilingi bilioni 9 ambapo kila mwaka shilingi bilioni 3.

Ligi Kuu ya Tanzania Bara sasa itafahamika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)

Rais wa TFF Wallace Karia akizungumza katika hafla ya utiaji saini amesema Udhamini huo utaleta matokeo chanya na watatoa ushirikiano kwa muda wote wa Mkataba.

Amesema Uendeshaji wa Mpira wa Miguu una gharama kubwa,wanawakaribisha Vodacom kushirikiana na wadhamini wengine.

Rais Karia ameongeza kuwa Kuongezeka kwa idadi ya timu kwenye mashindano ya CAF kufikia 4 ni kielelezo tosha cha kuimarika kwa Ligi Kuu.

Mkurugenzi wa Vodacom Hisham Hendi amesema ni furaha kubwa kuingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Hendi amesema Katika mipango yao ni kuona siku moja Watazamaji wanaoingia Uwanjani wanapata urahisi wa kununua tiketi kupitia huduma ya Mpesa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameipongeza TFF kwa hatua ya kusaini Mkataba na Kampuni ya Vodacom kudhamini Ligi Kuu.

Amesema Vodacom wameona uendeshaji bora wa TFF ambayo inaaminika na wanaingia katika moja ya Ligi Bora duniani.

Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika Makao Makuu ya Vodacom Plc.