Timu nane zatinga hatua ya robo fainali Ligi Daraja la Kwanza Wanawake
Timu nane kati ya Kumi na sita zilizokuwa zinashiriki Ligi ya wanawake Daraja la Kwanza zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika ligi hiyo inayoendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Fountain Gate Arena mkoani Dodoma.
Timu hizo ni Bilo FC ( Mwanza), Mkwawa Queens (Iringa), Mount Hanang (Manyara), Ruangwa Queens (Lindi), Mwanga City Queens ( Kigoma), Mlandizi Queens (Mlandizi), Sayari womens ( Dar es salaam) pamoja na mwenyeji timu ya Gets Program kutoka Dodoma.
Michezo hiyo ya hatua ya robo fainali itachezwa juni 17, 2024 katika uwanja wa Fountain Gate Arena ambapo timu ya Bilo FC itacheza dhidi ya Ruangwa Queens majira ya saa mbili kamili asubuhi, Mount Hanang dhidi ya Sayari womens majira ya saa nne kamili kamili asubuhi.
Mchezo mwingine utakuwa Kati ya Gets Program dhidi ya Mwanga City na mchezo wa mwisho utachezwa saa 10 jioni ukizikutanisha timu ya Mlandizi Queens na Mkwawa Queens.
Wakati huo huo timu 8 zimeaga mashindano hayo ambazo ni, JMK Park (Dar es Salaam), Ukerewe Queens ( Mwanza), Singida warriors ( Singida), Mpaju Queens ( Mbeya), Masala Princess ( Dar es Salaam), The Tiger Queens ( Arusha), Mapinduzi Queens (Njombe) pamoja na Oysterbay Girls ya jijini Dar es salaam.