Timu Nne WRCL Zapanda Daraja

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kwa Wanawake inayoendelea jijini Mwanza imefikia hatua ya nusu fainali ambapo timu nne zilizofuzu hatua hiyo zote zimefanikiwa kuvuka daraja, hivyo msimu ujao zitakwenda kushiriki ligi daraja la kwanza (Women First Division League).

Timu nne zilizo panda daraja ni; Mwanga City Queens (Kigoma), Gets Programm (Dodoma), Mpaju Queens (Mbeya) na Sayari Woman (Dar es Salaam).

Hata hivyo, timu hizo zitacheza mechi za nusu fainali Julai 25, 2023 kwenye uwanja wa Nyamagana. Mchezo wa kwanza utakaozikutanisha Mpaju Queens na Gets Programm utachezwa majira ya saa 7:30 mchana.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utapigwa majira ya saa 10:00 jioni kati ya Mwanga City na Sayari Woman, ambapo licha ya matarajio ya wadau wengi kuwa itakuwa ni michezo migumu bado makocha wote wamesema wamejipanga kuwakabili vyema wapinzani.

Ikumbukwe matokeo ya mechi hizo ndio yataamua watakao kutana kwenye fainali Julai 27, 2023.