Timu ya Taifa “Taifa Stars” inashuka dimbani leo kwenye dimba la El Merriekh,Omdurman kucheza dhidi ya Sudan mchezo wa marudiano kutafuta tiketi kufuzu CHAN.

Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa Taifa Stars kupata ushindi utakaowapa nafasi ya kuvuka.

Kuelekea mchezo huo Taifa Stars imecheza mchezo wa Kirafiki kwenye tarehe za Kalenda ya FIFA dhidi ya Rwanda uliochezwa Kigali,Rwanda Oktoba 14,2019 na kutoka suluhu 0-0.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti imetua Sudan tokea Jumanne na kuendelea kujifua kuelekea mchezo huo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amewataka Watanzania kuwa nyuma ya Televisheni zao ikiwa ni moja ya ishara ya kuwaunga mkono katika pambano hilo.

Amesema kila mmoja kwa imani yake vyema akaiombea Taifa Stars ili kuibuka na ushindi.

Katika mchezo wa Kwanza Sudan walipata ushindi wa goli 1-0 Uwanja wa Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Taifa Stars