Timu ya Taifa ya “Beach Soccer” yaanza kujinoa tayari kuikabili Burundi

Kikosi cha timu ya Taifa ya soka la ufukweni (Beach Soccer) kinachonolewa na kocha mkuu Boniphace Pawasa kimeingia kambini leo hii machi 8, 2021 na tayari kimeanza mazoezi katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam ili kujinoa kwa ajili ya  michezo miwili dhidi ya Burudi ambayo itawapa tiketi ya  kufunzu kucheza mashindano ya  AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwezi Mei, 2021 huko nchini  Senegal.

kocha Boniphace pawasa amesema kwamba mandalizi  yanaendelea vizuri mpaka sasa ikiwa leo ni siku ya nne tangu kuanza kwa mazoezi ya kujiweka sawa nje ya kambi  hivyo anamini watafanya vizuri katika mchezo ho ulio mbele yao dhidi ya Burundi ambao unatarajiwa kupigwa Machi 30, 2021 katika fukwe za Coco jijini Dar es salaam na baadae mchezo wa marudiano utakaochezwa tarehe 3/04/2021 Katika uwanja huo huo.

Kwa upande wa nahodha wa timu hiyo Jaruph Juma alisema kwamba yeye pamoja na kikosi chake wamejiandaa kikamilifu na wako tayari kuyapokea maelekezo ya mwalimu na kuyafanyia kazi ili waweze kupata matokea mazuri. Zaidi ya hapo aliwataka wadau ,wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla kuwapa ushirikiano wa hali na mali pale inapohitajika ili kikosi kizidi kuimarika na kupata hamasa ya mchezo.

Timu ya taifa ya Tanzania ya  Soka la Ufukweni (Beach soccer) inashikilia nafasi ya 7 kati ya timu 30 bora barani Africa.