Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali za Africa zitakazofanyika nchini Misri.

Timu ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali hizo baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha barua ya kujiondoa katika mashindano.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tayari wametujulisha taarifa hiyo ya kufuzu kucheza Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi Nane.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni ilikuwa kambini kujiandaa na mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili Septemba 9,2018.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.