Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys na Timu ya Taifa ya Vijana U20 “Ngorongoro Heroes” zimeondoka kuelekea Rwanda na Eritrea.

Serengeti Boys wapo nchini Rwanda na Kikosi cha Wachezaji 23 na viongozi 8 kushiriki mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon ya Vijana U17 itakayofanyika Tanzania Aprili 14-28,2019.

Mashindano hayo maalumu ya Kimataifa yatajumuisha timu 3 Serengeti Boys,Cameroon na wenyeji Rwanda ambapo kila mmoja atacheza na mwenzake.

Yanatarajia kuanza Machi 28-Aprili 4,2019 Kigali,Rwanda.

Kikosi cha Ngorongoro Heroes wenyewe wapo Asmara Eritrea watakapocheza mchezo wa Kirafiki na Eritrea Machi 31,2019 nchini humo.

Jumla ya Wacheza 20 na Viongozi 8 wapo katika msafara huo.

TIMU YA TAIFA U18 YAINGIA KAMBINI

Kikosi cha Timu ya Taifa U18 kimeingia Kambini kujiandaa na mashindano maalumu yatakayofanyika nchini Misri kuanzia Aprili 4-14,2019.

Mashindano hayo yatashirikisha nchi za Morocco,Algeria,Tanzania na wenyeji Misri.

Kikosi hicho kitaanza mazoezi kesho