Timu ya Taifa ya Vijana ya Wanawake U20 “Tanzanite” inaendelea kujiandaa na mashindano ya COSAFA yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.

Kikosi cha Wachezaji 29 kipo Kambini Shule ya Filbert Bayi Kibaha ikifanya maandalizi asubuhi na jioni.

Leo Kikosi hicho kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume,Ilala.

Kocha Mkuu Bakari Shime amesema maandalizi yanaendelea vyema katika nia ya kwenda kuleta ushindani kwenye mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia Agosti 1 mpaka Agosti 11,2019.

Shime anasaidiwa na Edna Lema,Kocha wa makipa Fatuma Omary,Meneja Vifaa Ester Chaburuma na Daktari wa Timu Blandina Mnambya.