“Tumejiandaa Kuhakikisha Tunamtoa Katika Njia” Samatta

Kauli ya Samatta kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON Machi 24,2023 Taifa Stars dhidi ya Uganda ikiwa ni sehemu ya maneno yake akielezea namna ambavyo wachezaji walivyojiandaa kuwakabili wapinzani wao.

Nahodha wa Stars Mbwana Samatta alisema kuwa mpinzani wao wanamfahamu vizuri kutokana na usumbufu ambao huwa anaonyesha kila anaposhiriki mashindano na kwamba wako tayari kumdhibiti asionyeshe makali yoyoye mbele yao.

“Pambano ni kumjua mpinzani wako, hivyo licha ya kumjua Uganda kuwa ni mgumu kupata matokeo kwake ila sisi tumejiandaa kuhakikisha Tunamtoa  katika njia kwasababu mafanikio ya kwenda kwenye michuano ya Afrika yanaanzia kesho.”Alisema Samatta

Aidha Samatta alisema kuwa imani yao kubwa ni kupata matokeo kwenye michezo yote miwili wakianza kubeba tatu za Misri na baadae kumaliza hesabu Benjamin Mkapa.

Wakati Samatta akiyasema hayo kwa upande wa kocha mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche mwenyewe amewahakikishia watanzania kuwa anakikosi bora na kizuri anacho kiamini, na kwamba wako tayari kupambana kupata ushindi na hatimae kufuzu kushiriki fainali hizo hapo baadae.