Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

MOROCCO : TUPO TAYARI KUWAKABILI NIGERIA

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanaume wenye umri chini ya miaka 23 (U23), Hemed Morocco amesema wapo tayari kuwakabili Nigeria kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Morocco alisema licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali bado ana kikosi kipana kitakachoingia kusaka matokeo chanya.

Aidha amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwapa hamasa zaidi ya kupambana katika mchezo huo wa nyumbani.

Naye Ally Msengi akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake alithibitisha utayari wao na kwamba wataingia uwanjani kutafuta matokeo muhimu mbele ya Nigeria kutokana na maandalizi mazuri waliyoyapata kutoka kwa benchi la ufundi.

Alisema wachezaji wengi wana uzoefu na mashindano makubwa hivyo watahakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Kufikia hatua hiyo Tanzania iliwaondoa Sudan Kusini wakitoka suluhu 0-0 kwenye mchezo wa kwanza na mchezo wa marudiano ukimalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.