Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Twiga stars kukutana na Namibia michuano ya Cosafa

Timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ itakutana na timu ya taifa ya Namibia katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Hollwoodbets Cosafa women’s championship inayoendelea kutimua vumbi Port Elizabeth nchini Afrika kusini.

Twiga stars imeangukia hatua hiyo baada ya kupoteza katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Zambia kwa bao 2-1 huku mwenyeji Afrika kusini akipata ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia.

Mchezo huo wa nusu fainali ulipigwa majira ya 6:00 mchana kwa saa za Port Elizabeth, Zambia wakipata bao dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji (JN: 11) Barbara Banda na kuwafanya twiga stars kuamka na kuongeza mashambulizi kitendo kilichopelekea beki wa Zambia Agness Musese kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.

Kikosi cha Zambia kilionekana kutaka kulipa kisasi cha kufungwa na Twiga Stars katika nusu fainali za mashindano hayo mwaka jana. Kipindi cha pili Zambia walianza kwa kasi na kufanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 46 likifungwa na Chisha Misozi (JN:7) lakini hata hivyo Twiga Stars waliendelea kucheza mchezo mzuri na wa kiufundi ila bahati haikuwa yao.

Akizungumzia mchezo huo kocha Bakari Shime alisema mchezo ulikuwa mzuri bila kujali matokeo na ilikua ni kipimo sahihi kwa kikosi cha ‘Twiga Stars’ kwasababu wamekutana na timu bora na inayocheza mashindano makubwa ya kombe la dunia. Kwa upande mwingine imewapa uzoefu baadhi ya wachezaji wa ‘Serengeti Girls’ waliojumuishwa katika kikosi wanaojiandaa kwa mashindano ya kombe la dunia mwezi Oktoba.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.