Twiga Stars Mabingwa Tunis Women’s Cup

Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” imetwaa Ubingwa mashindano ya Tunis Women’s Cup 2024 yaliyofanyika nchini Tunisia yakishirikisha nchi za Tanzania, Botswana na wenyeji Tunisia.

Twiga Stars ilifikia kutwaa Ubingwa huo baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka suluhu kwenye mchezo mmoja ikifikisha jumla ya alama 4 ambazo hazijafikiwa na timu yoyote, vile vile timu hiyo ndiyo pekee ilifunga magoli mengi zaidi Kwa odadi ya magoli 5 kwenye mashindano hayo.

Sambamba na hayo pia Twiga Stars ndio timu pekee iliyo iliyotowa mchezaji aliyepiga hat trick kwenye mashindano (Aisha Juma), matokeo ambayo yatakuwa na faida kubwa Kwa upande wa vigezo vya FIFA katika upande wa kupanda na kushuka Kwa viwango vya soka Kwa Nchi hususani Kwa upande wa soka la wanawake.

Baada ya kutwaa Ubingwa huo kocha Mkuu Bakari Shime aliwapongeza wachezaji wake na kusema wamefikia asilimia 100% ya malengo yao kwenye mashindano hayo, huku akisisitiza huo ni muendelezo wa kukiimariaha zaidi kikosi chake Kuelekea mashindano yaliyokuwa mbele yao.

Hata hivyo licha ya wenyeji Tunisia kukubali kipigo kikubwa Kwa Tanzania haikuwa timu rahisi kifungika kwenye mchezo dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa Julai 15, 2024 uliomalizika Kwa Tunisia kubeba alama 3 na matokeo ya ushindi wa goli 1-0.

Kwa matokeo hayo baada ya Mabingwa Tanzania (Twiga Stars), timu iliyomaliza nafasi ya pili ni ya wenyeji Tunisia huku Botswana ikimaliza nafasi ya

tatu.