Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Twiga Stars yatinga nusu fainali Cosafa

Timu ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ imefanikiwa kusonga mbele hatua ya nusu fainali katika michuano ya Hollywoodbets Cosafa women’s championship baada ya kuiondosha timu ya Malawi kwa bao 3-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua za makundi uliopigwa leo Septemba 07, 2022.Mchezo huo ulikua wa muhimu sana kwa timu zote mbili kwani ndio ungeamua nani asonge mbele na nani abaki, lakini ilikuwa ni Twiga Stars iliyoibuka kidedea katika mchezo huo. Kwa upande mwingine ulikua mchezo wa kisasi kwa timu ya Malawi wakitamani kuifunga ‘Twiga Stars’ baada ya kukatisha safari yao ya kutwaa ubingwa mwaka jana.Donisia Minja ndiye aliyeandika bao la kwanza kwa ‘Twiga Stars’ dakika ya 20 huku Diana Msemwa akipachika bao la pili dakika za nyongeza kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili ‘Twiga Stars’ walirejea kwa kasi wakiongeza mashambulizi katika lango la Malawi na kupelekea nyongeza ya bao la tatu lililofungwa na Opa Clement. Timu ya Malawi iliambulia bao moja la kufuatia machozi kutoka kwa mchezaji JN 07 Asimenye Simwaka Dakika 64 na Ireen Khumalo akikosa penati dakika ya 82. Baada ya mchezo kumalizika Nahodha wa Twiga Stars’ Amina Bilal alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo. Twiga Stars watakutana na Zambia katika nusu fainali itakayopigwa Septemba 09,2022 katika Dimba la Isaac Wolfson , mchezo wa pili wa nusu fainali utawakutanisha timu Mwenyeji Afrika kusini ‘Banyana Banyana’ dhidi ya Namibia.Wakati huo huo timu ya Botswana imeaga mashindano Kibabe kwa kuichakaza Comoro kwa bao 6-0 katika mchezo wa mwisho wa kundi C uliopigwa katika dimba la Madibaz na kuacha historia ya kutokufungwa na timu yoyote. Timu nyingine zilizoaga mashindano hayo ni pamoja Malawi, Msumbiji, Mauritius, Angola, comoro, Eswatini na Lesotho.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.