Twiga Stars yawasili Botswana

Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Leo Oktoba 28,2023 imewasili nchini Botswana tayari kwa mchezo wa marudiano wa kufuzu Olimpiki dhidi ya Botswana utakaochezwa Oktoba 31, 2023 katika uwanja wa taifa, Gaborone (Botswana).

Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini Botswana Kocha mkuu wa Twiga Stars Bakari Shime alisema, kikosi kimewasili salama nchini Botswana na wachezaji wote wako katika hali nzuri hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza tangu timu inatoka nyumbani Tanzania mpaka inawasili Botswana.

” Tunashukuru kwa mapokezi mazuri tuliyoyapata kutoka kwa Maafisa Ubalozi wa Pretoria, hii inaonyesha kwamba serikali iko pamoja na sisi na inatambua umuhimu wa mchezo huu hivyo tuna kazi kubwa ya kuhakikisha timu inapata ushindi ili tuweze kusonga mbele katika hatua inayofuata na watanzania wote wafurahi na kujivunia nchi yao”. alisema Kocha Shime

Katika mchezo wa awali raundi ya pili  Tanzania ilipata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Botswana katika uwanja wa Azam Complex Chamazi. Mchezo huo ulichezwa Oktoba 26, 2023.