Mechi kati ya Uganda na Malawi imemalizika hivi punde na Uganda kuchukua pointi tatu baada ya kuitungua Malawi kwa mabao 6-5.
Mabao yaliyoipa ushindi Uganda yamefungwa na Wasswa Emmanuel alietupia wavuni mabao matatu huku mengine ykifungwa na Somoka Rowch, Lwesibawa Godfrey na Muganga Douglas.
Magoli ya Malawi yamepachikwa na Sandam Said, James Chikoka, Vanancio Malunga na Isaac Kajamu aliyefunga mabao mawili.
Kutokana na matokeo hayo, Uganda imefikisha pointi saba na kuongoza wakati Malawi imemaliza michuano bila pointi baada ya kufungwa mechi zote.
Baada ya mchezo huo, mechi itakayoanza hivi punde ni kati ya bingwa mtetezi Tanzania na Burundi ambao wote wanaingia wakiwa na alama 6 na magoli 17.
Mchezo huo ndio utakao amua bingwa wa michuano ya COPA DAR ES SALAAM leo.