Ujenzi wa Kituo cha Kukuzia Vipaji vya Mpira wa Miguu na Viwanja Kigamboni na Tanga Kuanza Rasmi Oktoba, 2020.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Wallace Karia amewakabidhi kampuni ya Group Six International eneo la ujenzi hii leo 29 Septemba, 2020
Kigamboni, Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi wa miradi hiyo miwili inayotarajiwa kutekelezwa na TFF kuanzia Oktoba mwaka huu.
Tukio hilo la makabidhiano rasmi limefanyika majira ya ya saa tano asubuhi ikiwa ni siku chache tu mara baada ya tukio kama hilo kufanyika huko Jijini Tanga siku ya Jumamosi ya tarehe 26 Septemba, 2020.
Makabidhiano hayo yalishudiwa na viongozi mbalimbali wa TFF wakiongozwa na Rais Wallace Karia ambaye ndiye aliyekabidhi eneo hilo kwa makandarasi wa ujenzi wa kituo cha michezo cha Kigamboni technical center.
Akizungumza kwa furaha wakati wa makabidhiano hayo Rais Karia alisema: “tunayo furaha kubwa mpaka kufikia hatua hii, haya ni makabidhiano kama yale tuliyo yafanya Tanga japo hapa Kigamboni tumeona hakuna changamoto kubwa kutoka kwa wakazi kama ilivyo katika eneo letu la Tanga na kwamba eneo hili la Kigamboni liko vizuri lakini changamoto kubwa ni umeme tu, japokuwa tuko kwenye mchakato wa kumalizia hilo,na muda sio mrefu ujenzi utaanza rasmi’’. Alisema Rais Karia huku akitabasamu kwa bashasha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Group Six International Mr Janson Huang alisema kuwa ‘ Kampuni yao ni moja ya kampuni bora ya ujenzi nchini Tanzania na wameihakikishia uongozi wa TFF kuwa ujenzi huu utamalizika ndani ya muda walio kubaliana na tena kwa ubora wa hali ya juu zaidi.
” Tunahakika na kazi zinazofanywa na kampuni yetu ya Group Six International katika masuala ya ujenzi kwani kampuni yetu imekuwa ni moja kati ya makampuni Bora ya ujenzi hapa nchini Tanzania, hivyo hatuna shaka kwa kuwa tunaamini kazi hii itamalizika kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati tuliokubaliana”. Alisema Jonson Huang.
Ujenzi huo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Octoba 2020 na unatarajiwa kuchukua muda wa mwaka mmoja mpaka kukamilika kwake; pia ujenzi huo unatarajia kutengeneza ajira na fursa nyingi kwa wakati wa maeneo husika na kutoka sehemu nyingine nchini Tanzania.
Viongozi wengine waliokuwepo kwenye tukio hilo ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Ndugu, Cornel Barnabas, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani na Uzingatiaji Ndugu, Hassan A. Njama