Serikali Yaimwagia Sifa TFF kwa Usimamizi Mzuri wa Soka Nchini
Serikali imelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuendelea kusimamia vizuri maendeleo ya Mpira wa Miguu nchini kutokana na mafanikio makubwa yalipatikana chini ya Rais wa TFF Wallace Karia, tangu kuingia kwake madarakani 2017.
Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa kwenye hafla ya ugawaji wa TUZO za TFF iliyofanyika Agosti 1, 2024 katika Ukumbi wa Super Dome, uliopo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Akielezea zaidi kuhusu mipango ya Serikali kulipeleka mbele soka, pamoja na michezomingine nchini, Mhe.Msigwa alisema kuwa Serikali inaendelea kutenga fungu kwa ajili ya kuusukuma michezo zaidi kwani inafahamu kwamba michezo ni ajira na ni afya pia, hivyo inapaswa kuendezwa kwa kushirikiana na wadau huku akitoa mwito kwa wadau wengi kujitokeza kudhamini michezo ikiwa ni pamoja na kuwalea kwa ueledi wanamichezo hao ili wasipotee.
Aidha, Mhe. Msigwa hakusita kuipongeza Azam Media Ltd., kwa kuwekeza zaidi kwenye kuionesha michezo (soka) nchini. Aliisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umekusudia kuendelea kuungua mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa soka nchini hasa TFF kuhakikisha maendeleo makubwa zaidi yanapatikana.
Akihitimisha hotuba yake fupi, Mhe. Msigwa alisisitiza wadau wengi zaidi kuendelea kuwekeza kwenye michezo, akitabaisha kuwa vipaji bila taaluma haviwezi kwenda mbali, na matokeo yake hufia njiani Kwa kukosa maarifa ama taaluma. Hivyo, kuwataka wadau kujitokeza katika kuisaidia Serikali na TFF kwenye Elimu ya michezo kwani michezo ikifundishwa vizuri inalipa.
Akiwakaribisha wageni katika hafla hiyo Mwenyeji wa tukio hilo, Rais wa TFF Wallace Karia alisema kuwa utoaji wa TUZO umekuwa ukibadilika kutokana na mahitaji ya wakati pia. Karia aliongeza kuwa kubadilishwa huko kwa utoaji wa TUZO kumezingatia kuongeza nafasi ya upatikanaji wa washiriki wengi zaidi, hasa wale wanaopata TUZO hizo; kwani kusogezwa mbele kwa hafla hiyo pia kumetoa fursa kwa wachezaji wengi zaidi kuweza kuhudhuria.
Karia aliongeza akisema kuwa utoaji wa TUZO utakuwa ukiboreshwa kulingana na mahitaji ya wakati; kwani msimu huu kunamaboresho kadhaa yamefanyika tofauti na msimu ulikopita, lakini msimu ujao utakuwa na maboresho makubwa zaidi ambapo utagusa maeneo mengine kama vile shabiki bora na timu iliyoingiza mashabiki wengi zaidi kwenye msimu husika.
Katika Zoezi la ugawaji wa TUZO wachezaji mbalimbali waliibuka na TUZO ambapo kwenye michuano ya Shirikisho ya Kombe Benki ya CRDB; Clement Mzize alichukua TUZO ya ufungaji bora, Djigui Diarra akiibuka na ya golikipa bora na Azizi Ki kiungo bora wote kutoka Young Africans, huku Feisal Salum akiibuka mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho. Ligi Kuu ya Wanawake Aisha Juma Mnunka aliibuka mfungaji bora na mchezaji bora pia