Uzinduzi rasmi wa programu ya mpira wa miguu kwa shule (Football For Schools- F4S) utafanyika Jumatatu, 15 Aprili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 

Shughuli ya uzinduzi wa programu hiyo inayoendeshwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

 

Walimu 48 kutoka mikoa 16 ya Tanzania ambapo miongoni mwao 19 ni wanawake wanashiriki kwenye programu hiyo.

 

Programu ya F4S imelenga kuchangia elimu, maendeleo na kuwawezesha zaidi ya watoto milioni 700 duniani.

 

Kupitia programu hiyo, wavulana na wasichana watafurahia mpira wa miguu kwa vile mchezo huo utaingizwa katika mfumo wa elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.