Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF limewateua waamuzi kutoka Tanzania kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Nasr Athletic ya Algeria dhidi ya Green Eagles ya Zambia utakaochezwa Disemba 21, 2018.
Katika mchezo huo Mfaume Ali Nassoro atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Ferdinand Chacha, Mwamuzi msaidizi namba 2 Salim Mkono Mohamed na Mwamuzi wa Akiba Alphonce Mwandembwa.
Kamishna wa mchezo huo anatokea Misri Karam Kordy Abel Fattah