Waamuzi RCL Kunolewa Makao Makuu TFF

 

Kozi ya siku tano kwa waamuzi wa ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL 2024) inaendelea makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Kozi hiyo inayojumuisha washiriki 107 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania, imeanza Machi 1, 2024 kwenye uwanja uliopo makao makuu ya TFF Karume Ilala Dar es Salaam katika eneo la kuwapima washiriki hao eneo la utimamu wa mwili kwa kufanya mazoezi ya vitendo.
Wakufunzi wanao simamia mafunzo hayo ni; Soud Abdi mkufunzi wa ufundi, Israel Mjuni, pamoja na Samwel Mpenzo ni wakufunzi kwa upande wa utimamu wa mwili.
Ikumbukwe mwishoni mwa kozi hiyo ni baadhi ya wahitimu watakao faulu ndio watachaguliwa kuchezesha mechi hizo kwenye vituo vitakavyo tumika kwa mechi za ligi hiyo kuanzia hatua ya mikoa.