Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

 

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia amewataka waandishi wa habari za michezo hususani mpira wa miguu kuhakikisha wanatumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kuandika habari zenye tija ambazo zitachangia kukuza soka la Tanzania.Hayo ameyasema leo Agosti 27,2022 alipokuwa akihitimisha semina ya siku moja kwa waandishi wa habari za michezo iliyofanyika katika hoteli ya Tiffany Diamond iliyopo maneno ya posta jijini Dar es Salaam.Rais wallace Karia aliwasisitiza waandishi kuepuka kuandika habari zenye mgongano na ambazo hawajazifanyia utafiti wa kina, jambo ambalo litashusha weledi wa mwandishi na kuharibu taswira ya chombo cha habari husika. ” Tunawapa mafunzo haya ili kuwaongezea ujuzi katika utendaji wa kazi zenu, mitandao ya kijamii ina manufaa makubwa na wengi mmepata ajira kupitia huko, jitahidini kuitumia vizuri kwa kuweka taarifa zilizo sahihi ili hata wanaosoma waone kweli hawa waandishi wana weledi na wanajua wanachokifanya. Shirikisho linawategemea kufikisha habari za soka zilizo sahihi kwa watanzania hivyo mzingatie hilo”.Semina ilihitimishwa kwa washiriki 54 kutoka vyombo mbali mbali vya habari kukabidhiwa vyeti vya ushiriki na Rais wa TFF, huku mkufunzi wa semina hiyo Andrew Oryada kutoka Uganda akisema amefurahishwa na mwitikio wa waandishi wa habari na namna walivyoshiriki katika kuchangia mada zilizotolewa.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.