Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) , Wallace Karia akiambatana na wajumbe wa kamati ya ukaguzi na udhibiti hii leo May 7, 2021 kukagua mradi wa TFF ulioko Kigamboni, Dar es Salaam.
Mradi wa Kigamboni ni moja kati ya miradi mikubwa inayo tekelezwa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ikishirikiana na FIFA ukiachilia mbali mradi mwingine unao endelea mkoani Tanga hii yote ikiwa ni utekelezaji bora wa uongozi wa TFF .
Aidha Rais , Wallace Karia aliwaelezea wajumbe hao umuhimu wa mradi huu na kusema “ Mradi huu utaleta faida sana kwetu kwani kila mwaka hutumia pesa nyingi kwenye mashindano kulaza watu lakini mradi huu utakuwa na mabweni kwaiyo vijana walala hapa hapa hivyo tutaokoa pesa nyingi na tunaweza pia kuingiza pesa” alisema Karia.
Huku kwa upande wa mhandisi msaidizi wa ujenzi , Sylvester Mbawala akieleza toka ujenzi ulivyoanza Oktoba 24, 2020 mpaka sasa hatua za ujenzi za mradi wa Kigamboni umefikia asilimia 25% licha ya changamoto za mvua kufanya baadhi ya vitu kwenda taratibu lakini mpaka kufikia Octoba 23, 2021 inatarajiwa mradi kuwa umesha malizika.