Wajumbe wa kamati ya ukaguzi na udhibiti wakikagua mradi wa TFF ulioko Tanga May 08 2021, Katika eneo la mradi Donge, Tanga.

Baada ya kumaliza zowezi la ukaguzi wa mradi ulioko kigamboni, Dar es Salaam May 07, 2021 wajumbe hao wamendelea na zoezi la ukaguzi katika mradi mwingine ulioko chini ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania chini ya uwezeshwaji kutoka FIFA uliko Donge mkoani Tanga.

Aidha mhandisi msaidizi wa ujenzi , Omary Mozart alieleza toka ujenzi ulivyoanza Oktoba 24, 2020 mpaka sasa hatua za ujenzi za mradi wa Tanga umefikia hatua kubwa sana licha ya changamoto mbalimbali kama vile mvua kubwa kufanya baadhi ya vitu kwenda taratibu lakini mpaka kufikia Octoba 23, 2021 inatarajiwa mradi kuwa umesha malizika.

Kwa upande wa Mkaguzi wa ndani na mdhibiti wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) , Hassan Njama ameupongeza uongozi mzima wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kuwawezesha wajumbe hawa kutekeleza ukaguzi huu kwani ni jambo zuri kwa afya ya maendeleo katika taasisi.