Yanga Yashinda Tena Uhuru, Yaipiga Ruvuma 2-0
Mchezo uliochezwa kati ya Yanga Princess na Ruvuma Queens ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-0 na kukifanya kikosi hicho kinachonolewa na Edna Lema kujiongezea alama tatu na kuzidi kujihakikishia kubaki katika ligi kuu ya Serengeti Lite.
Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru ulikuwa ni wa muhimu kwa kila timu kutokana na kila timu kutaka kupata ushindi ili kujihakikishia kubaki katika ligi hiyo ya wanawake.
Yanga walikuwa na presha zaidi kufuatia mwenendo mzuri wa wapinzani wao wa jadi Simba Queens ambao wako mbele kwa alama nyingi huku pia idadi ya magoli ikiwabeba zaidi. Yanga ilipata bao lake la kwanza katika kipindi cha awali, bao lililo
dumu mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko.
Mara baada ya kurejea kipindi cha pili Yanga walionekana kuzidi kulisakama lango la wapinzani wao, na kufanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa mchezaji Amina lly jezi namba 4. Mapaka dakika tisini (90) zinakamilika Yanga Princess ilitoka kifua mbele kwa idadi ya magoli mawili kwa sifuri.
Kocha mwenye mbwembwe nyingi Edna Lema (Mourinho) alisema kuwa kikosi chake kimecheza vema na kwamba anashukuru Mungu kwa ushindi huo walioupata na kuongeza kuwa atazidi kujipanga zaidi ili kuhakikisha anamaliza katika nafasi nzuri na ikibidi kuupata ubingwa pia endapo wapinzani wao watafanya uzembe na wakapioteza michezo mingi.
Koche Lema alieleza kuwa kikosi chake kinazidi kuimalika siku hadi siku na anaimani na kikosi hicho kwa kwamba bado kinajipanga zaidi ili nkizidi kufanya vema katika michezo mitano iliyosalia.
Naye kocha msaidizi wa Ruvuma Queens aliye jitambulisha kwa jina la Konyang’anya alisema kuwa mpira unamatokeo matatu kushinda, kushindwa na kusuluhu; huku akisema kuwa atajipanga vema kwa mchezo unaofuata kwani atakuwa nyumbani hivyo, atahakikisha anashinda katika michezo yote mitatu ya nyumbani na kupambania ile miwili ya ugenini.
Baada mchezo huo wa Yanga Princess na Ruvuma Queens timu hizzo zote zimebakiza michezo mitano ili kukamilisha ligi ya Serengeti Lite kwa msimu huu.