Mtanange wa mechi roundi ya nne kati ya Yanga Princess na Simba Queens unaendelea  katika uwanja wa Karume ambapo mpaka sasa Simba Queens anaongoza kwa goli 2-1………

Ni katika dakika ya 13 tatu tu ambapo nahodha wa timu ya Simba Queens jezi namba7; Mwanahamisi anafanikiwa kuipatia  bao la kuongoza; goli ambalo limedumu kwa dakika kadha, na mnamo dakika ya 25 ya kipindi hicho cha kwanza Mchezaji  wa Yanga Princess, jezi namba 14 mgongoni, Shelda Boniface anaisawazishia timu yake baada ya kuunganisha crosi kwa kichwa.

Mnamo dakika ya 35 Simba Queens inapata goli la 2 linalofungwa na mchezaji jezi 8 Neema Kininga ambalo limedumu mpaka timu hizo zikienda  kwenye mapunziko.

Mechi ni mapumziko, bado mahabiki wa timu hizi kubwa nchini wanasubiri kwa hamu nani ataibuka na pointi tatu muhimu hii leo.