Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Timu ya Wananchi (Yanga) Watakata na Kuwapoza Mashabiki, Yaitoa Azam Nafasi ya Pili

Mchezo kati ya Yanga na Singinda United Ulipigwa Leo 15 Julai 2020 na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-1 kisha kurejesha furaha Jangwani hasa baada ya kuiondoa Azam katika nafasi ya pili.

Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 1:00 usiku ulikuwa na purukushani za hapa na pale huku Yanga wakionesha kuusaka ushindi kwa nguvu ambapo wanajamgwani hao waliuanza mchezo kwa kasi wakihitaji bao la mapema zaidi.

Mnamo dakika ya 34 ya mchezo huo Yanga ilifanikiwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa Paul Godfrey, na katika daika ya 38 mchezaji mkongwe Mrisho Ngassa naye akagongelea msumari wa pili. Hata hivyo, Singinda nao hawakuridhika kutoka kapa katika kipindi hicho na hivyo kujituma na hatimaye kufanikiwa kupata bao mnamo dakika za majeruhi za kipindi hicho za kwanza, goli liliopachikwa na Stephen Sey na kuzifanya timu hizo kwenda kwenye mapumziko  zikiwa na tofauti ya bao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza na Singinda United wakianza kulisaka bao la kusawazisha. Wakati Singinda wakitafuta kusawazisha Yanga wao pia walikuwa wakisaka goli la tatu ili kujihakikishia ushindi na kushika nafasi ya pili iliyokuwa ikishikiliwa na Azam FC ambayo katika mchezo wake na Mtibwa Sugar tayari ilikuwa imekwisha lala kwa bao moja kwa sifuri.

Yanga waliongeza juhudi zaidi na kafanikiwa kupata bao kupitia kwa mchezaji Yikpe Gisilain aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi, na kubadili ubao wa matokeo na kuwa 3-1. Katika mchezo huo Yikpe alionekana kuwa na makeke huku akiwa na kasi na hamu ya kupata mabao zaidi jambo lililowafanya mashabiki wa Yanga kumshangilia kwa kumpigia makofi kila aliposhika mpira.

Hii ni agharabu sana kutokea, lakini hali ndivyo ilivyokuwa katika mchezo huo uliopigwa kwa Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinakamilika Yikpe alionekana kuwa kivutio kwa mashabiki wa Yanga; hii inasadifu msemo usemao “thamini ulichonacho na sio ukitakacho”.

Kocha wa kikosi cha Yanga Luc Eymael alikipongeza kikosi chake kwa ushindi huo wa bao 03 licha ya kutoridhishwa na kiwango kilichooneshwa na kikosi chake katika mchezo huo. Wakati Kocha wa Singinda United Ramadhan Nswanzurimo yeye alidai kuwa kikosi chake kilicheza vizuri licha ya kuwa tayari kimeshuka daraja na kuongeza kuwa mpira ulikuwa mzuri hata hivyo kikosi chake kina hali mbaya kiuchumi na hiyo ndio sababu kubwa ya kupata matokeo mabaya mara kwa mara.

Kikosi cha Yanga kilichoanza katika mchezo huo ni; Farouk Shikhalo, Paul Godfrey, Adeyun Saleh, Kelvin Yondan,  Lamine Moro, Abdul Azizi Makame, Mrisho Ngassa, Raphael Daud, Deusi Kaseke, David Molinga na Patrick Sibomana. Wachezaji wa akiba walikuwa;  Ramadhan Kabwili, Ally Mtoni, Jafar Mohamed, Erick Kabamba, Yikpe Gilslain, Ditram Nchimbi na Adam Kiondo.

Kwa upenda wa Singinda United wachezaji walioanza ni; Owen Chaima, George Wawa, Reward Mshanga, Kazungu Mashauri, Ertick Emmanuel, David Nartey, Seiri Arugumaho, Emanuel Simon, Styephan Sey, Stephen Opoku na Emanuel Manyanda. Wachezaji wa akiba walikuwa; Mkumbo Msafiri, Aldof Anthony, Ramadhan Hashim, Yazidu Idd, Shabani Husein na Anjero Mbilinyi.

Kufuatia ushindi huo Yanga sasa inashikilia nafasi ya pili kwa kujikusanyia jumla ya alama 64 ikiwa mbele ya Azam kwa alama 2, kwani alama za Azam kabla ya mchezo wa mwisho aliofungwa alikuwa na alama zake 62.

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.