Young Africans Yaishusha Simba Kileleni

Timu ya Young Africans imefanikiwa kuwapiga wapiga kwata, Tanzania Prisons bao 1-0 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC wakiwaondoa Simba Sport Club iliyokalia usikani kwa huo kwa masaa kadhaa mara baada ya kupata Ushindi mnono kwenye mechi ya dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Disemba 03, Mkwakwani Tanga.

Mchezo huo kati ya Young Africans na Tanzania ulipigwa Disemab 04, 2022 majira ya saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Tanzania Prisons licha ya kuwa ugenini walifanikiwa kuwadhibiti wenyeji hao kwa dakika 88, baadaye mnamo dakika ya 89,ulinzi ulivurugwa baada ya Feisal Salum (Fei Toto) kupachika bao pekee lililowapeleka Prisons nje wakiwa vichwa chini.

Bao hilo la Feitoto lilipatikana kutokana na usumbufu alioingia nao Benard Morrison (BM 33) dakika za mwisho ambaye alionekana kuwatia presha zaidi walinzi wa Tanzania Prisons hatimaye kukubali yaishe.

Kocha msaidizi wa Young Africans Cedric Kaze alisema kuwa mchezo huo ilikuwa mgumu kutokana na ubora wa Tanzania Prisons katika kulinda na kufanya mashambulizi makali yavkushtukiza jambo ambalo liliwapa ugumu wachezaji wake na kuwafanya watabike kwa dakika zote 88 bila bao. Kaze aliendelea kusema kwamba ushindi huo walioupata utawafanya Young Africans kwenda katika mchezo wao wa mwisho wa duru ya kwanza unatarajiwa kuchezwa dhidi ya Namungo FC, wakijiamini jambo ambalo litawaongezea utulivu kwa kuwa watakwenda wakiwa vinara wa ligi.

Naye kocha wa Tanzania Prisons Patrick Odhiambo alisema mchezo huobulikuwa na peesha kubwa kwao na kwamba mpango walioingia nao kwanza ni kuwaheshimu Young Africans kutokana na ubora wa kikosi chao pamoja na kuwa na wachezaji wenye viwango vizuri kwa moja moja. Aliongeza kuwa wachezaji wake walilifanya jutahada kubwa kuhakikisha wanatoka na alama yeyote lakini mpango huo ulivurugwa na timu hiyo yenye makazi yake Mitaa ya Twiga Kariakoo Dar es Salaam.

Hata hivyo, kocha Odhiambo aliwapongeza Young Africans kwa kuipambania timu yao kwa udi na uvumba na kuhakikisha wanapata matokeo hata kwenye wakati mgumu kama ilivyokuwa kwenye mchezo huo.

Baada ya mchezo huo Young Africans anarejea rasmi kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC wakicheza mechi 14 huku wakifanikiwa kukusanya jumla ya alama 35; alama moja mbele ya Simba wakati huo huo wao wakiwa na mchezo mmoja mkononi watakao kwenda kucheza na Namungo FC kwenye uwanja wa Kasimu Majaliwa Ruangwa Lindi.