Young Africans Yatangulia Fainali Kwa Kishindo
Fainali za ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka ishirini (U20) 2021 zimendelea hii leo June 14, 2021 kwa michezo miwili iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex , Dar es Salaam.
Mchezo wa kwanza uliwakutanisha Young Africans U20 dhidi ya Mwadui FC U20 lakini dakika za mapema tu Young Africans wakatangulia kupata goli kupitia Abby Mikimba dakika ya 12 na Abdukarimu Yunus dakika ya 44 na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa matokeo ya 2-0.
Kipindi cha pili Young Africans walirudi kwa kasi na haikuchukua dakika nyingi Abdukarimu Yunus akarudi tena kambani mnamo dakika ya 48 licha ya Mwadui FC kufanya umiliki mkubwa wa mpira lakini wakambulia kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa
vijana wa Young Africans.
Baada ya mchezo kocha wa timu ya Mwadui FC, Fred Masombola aliwapongeza wapinzani wake kwa kuweza kupita kwenye kundi A lakini hakusita kuwapongeza wachezaji wake kwa kujituma katika michezo yote na kuwasihi washabiki wa Mwadui kutokukata tamaa kwa timu yao.
Huku kwa upande wa mwalimu wa Young Africans Said Maulidi alianza kwa kuwapongeza sana wachezaji wake na kusema “ Uzoefu na kujiamini ndio nguzo kubwa iliyofanya mpaka tumefikia hatua hii na hatutoishia hapa nia yetu kama timu ni kuhakikisha tunafika mbali zaidi”, alaisema Maulidi.
Mchezo unaofata ni baina ya wekundu wa msimbazi Simba FC dhidi ya vijana kutoka JKT Tanzania U20 majira ya saa 3:00 usiku kwenya uwanja wa Azam Complex, Chamazi-Dar es Salaam.