Young Africans Yatangulia Fainali Ngao ya Jamii

Mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii 2022/2023 Young Africans wametangulia hatua ya fainali Ngao ya jamii baada ya kumpiga 2-0 Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza Agosti 9,2023 majira ya saa 1:00 usiku

Magoli mawili ya wachezaji Stephanie Aziz KI na kinda mshambuliaji Clement Mzinze yaliyopatika kipindi cha pili ndio yaliyoamua kuitanguliza timu hiyo fainali, kabla ya mchezo mwingine wa nusu fainali.

Young Africans itamsubiri mshindi kati ya Simba SC na Singida Fountain Gate wanaotarajia kukiwasha kwenye mchezo mwingine wa nusu fainali Agosti 10,2023.

Hata hivyo matokeo ya ushindi kwa Young Africans ni rekodi nzuri kwa kocha mkuu Gamondi ambae ameanza msimu kwa kupata ushindi dhidi ya Azam FC huku mpinzani wake Yusuf Dabo kocha wa Azam FC akipoteza kwenye mchezo wa kwanza.