Young Africans Yavunja Mwiko Kwa Mkapa, Simba Kujiuliza Kimataifa

Timu ya Young Africans imefanikiwa kupata alama tatu mbele ya Miamba ya Soka Africa, TP Mazembe kwenye mchezo uliopigwa Februari 19, 2023 katika uwanja wa Mkapa, majira ya saa 1:00 usiku.

Young Africans walifanikiwa kuandika bao la kuongoza mnamo dakika ya 7 ya mchezo kupitia kwa nyota wa Kimataifa Kennedy Msonda aliyejitusha Mpira nankuusukuma kambani kabla ya dakika chache Mdathir Abbas kuiandikia bao la pili lilozifanya timu hizo kwenda kwenye mapumziko ubao ukisomeka 2-0.

TP Mazembe iliamka katika kipindi cha pili na kupeleka mashambulizi mengi zaidi ambapo mnamo dakika ya 81 kipindi cha pili, walifanikiwa kuandika bao la kufuatia machozi kabla ya Tuisila Kisinda kukomelea msumari wa tatu kwenye dakika za lala salama, bao hilo likififisha matumaini ya Miamba hiyo kutoka Kongo kusawazisha.

Ushindi wa Young Africans unarejesha matumaini ya Watanzania kwamba uenda Yale yaliyofanywa na Simba Kwa miaka kadhaa yanaweza yakaendelezwa na Wananchi Msimu huu. Mpaka Sasa Young Africans wamecheza michezo miwili wakishinda mmoja na kupoteza mmoja ule wa ugenini uliochezwa 13 Februari, 2023 nchini Tunisia.

Wakati Young Africans wakifanikiwa kukusanya alama tatu na mabao matatu, kwa upande wa mwakilishi pekee Wa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba SC wameendelea kujiuliza baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mechi mbili mfululizo.

Simba ilikibali kupoteza nyumbani kwa magoli 3-0 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, kwenye mchezo uliochezwa Feb 18, 2023 uwanja wa Benjamin Mkapa huku ikishindwa pia kufunga bao lolote kwenye mechi zake hizo za kundi C na kuwafanya waburuze mkia.

Hata hivyo, Simba bado wanayonafasi ya kufanya vizuri endapo itafanya marekesho ya makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Raja Casablanca Februari 18, ambapo watatakiwa washinde michezo yote ya Nyumba ni huku wakitafuta sare moja na ushindi mmoja wa ugenini.

Mchezo unaofuata Simba watasafiri Hadi Uganda kuvaana na Vipers wakati Young Africans wao wataelekea Mali, kuwakabili AS Bamako yenye alama 1 pekee katika kundi lao baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya US Monastir.