Young Africans Yazidi Kung’ang’ania Nafasi ya Pili

Timu ya Young Africans imezidi kujikita katika nafasi yake ya pili baada ya kufanikiwa kuiadhibu Ruvu Shooting kwa jumla ya mabao 3-2 na kufikisha alama 64 na kuwafukuzia Simba ambao wao wana alama 67 huku wakiwa na michezo mitatu mkononi.

Mchezo huo uliopigwa katika ndimba la Mkapa majira ya saa 1:00 usiku ulianza kwa kusuasua kana kwamba hakuna timu iliyohitaji kupata matokeo; lakini baada ya dakika 15 kupita Young Africans waliamka na kuanza kulishambulia lango la Ruvu Shooting na kufanikiwa kutangulia kwa bao mbili kwa sifuri.

Feisal Salum (Fei Toto) akiiandikia timu yake bao la kwanza mnamo dakika ya 23 na baadae akirudi tena kumsalimu mlinda mlango wa Ruvu shooting Bidii Hussen(18) na kuiandikia bao la pili timu yake matokeo ambayo yalibaki hivyo mpaka dakika 45 zinakatika katika dimba la Mkapa.

Kipindi cha pili Ruvu Shooting walirudi kwa staili ya kuwapigisha kwata Young Africans na kupelekea madhara kwa mchezaji Mukoko Tonombe ambaye alipata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na mchezaji Said Ntibazonkiza (Antibiotic).

Baada ya dakika kadhaa kocha Charles Boniface Mkwasa(Master) alifanya mabadiliko yaliyoonekana kuzaa matunda(Super sub) alipo muingiza Emmanuel Martin(16) akitokea benchi ambaye aliandikia timu yake bao la kuongoza huku bao la pili likipachikwa na David Uromi mara tu baada ya dakika chache Young Africans walipopata bao la tatu. Kutoka kwa James Msuva diko kulimfanya Emmanuel Martin kuingia na kufungua milango ya magoli kwa Ruvu Shooting, yaliyoirudisha katika mchezo.

Supa sabu ya kocha Nabi, Said Ntibazonkiza ikikamilisha idadi ya mabao 3-2 matokeo yaliwafanya Young Africans kuendelea kusalia kwenye nafasi ya pili akiwa na alama zake 64 nyuma kwa alama 3 kutoka kwa vinara wa ligi hiyo Simba SC mwenye alama 67 kileleni.

Baada ya mchezo huo makocha wa vikosi vyote waliweza kuzungumzia mchezo huo. Kocha wa Young Africans Mohamed Nasreddine Nabi (double Ns) alisema kuwa kikosi chake kimecheza vizuri lakini ni makosa madogomadogo tu ndio yaliyopelekea wapinzani wao kuweza kupata bao mbili. Hata hivyo, bado wameweza kushinda.

Kwa upande wake kocha wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa yeye alisema kuwa walikosa bahati tu ya kupata ushindi licha ya kujituma na kufanya mashambulizi hasa kwenye kipindi cha pili. Mkwasa amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma lakini pia hakusita kuwapongeza Young Africans kwa wao kupambana pia na kupata ushindi huo huku akisema haikuwa rahisi kwa wao kuondoka na ushindi huo.

Aliongeza kuwa mchezo huo umewafungua macho na kubaini baadhi ya mambo ambayo watakwenda kuyafanyia kazi na kupata matokeo mazuri kwenye michezo mingine.

Kwa matokeo hayo Simba wanaendelea kuongoza ligi, Young Africans wakishika nafasi ya pili huku Azam wao wakisalia kwenye nafasi yao ya tatu.