Ruangwa Queens, Bilo zashuka daraja

    Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2025/2026 imemalizika rasmi tarehe 17 Juni huku timu za Ruangwa Queens ya Lindi na Bilo FC ya Mwanza zikishuka daraja.

    Simba Queens ndiyo iliyoibuka mabingwa baada ya kufikisha pointi 60 huku JKT Queens ikiwa makamu bingwa kwa pointi 52.

    Nafasi ya tatu imechukuliwa na Yanga Princess iliyofikisha pointi 50.

    Mashujaa Queens iliyokuwa kwenye vita kali na Fountain Gate Princesses imeendelea kuonesha ubora wake baada ya kumaliza kwenye nafasi ya nne, na kufanya kuwa sehemu ya timu zitakazocheza mechi za Ngao ya Jamii ambazo huzipa fursa timu nne za juu kwenye msimamo wa Ligi kuukaribisha msimu mpya.

    Matokeo ya mechi za mwisho ni; Simba Queens 3-0 Geita Queens, Alliance Girls 1-2 JKT Queens, Yanga Princess 2-0 Bunda Queens, Bilo FC 0-3 Mashujaa Queens, Fountain Gate Princesses 8-1 Ruangwa Queens na Ceasiaa Queens 2-1 Tausi FC.

    Share.