32 waitwa Twiga ya WAFCON

    Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), Bakari Shime leo Juni 18 ametaja kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wanawake (WAFCON) zitakazofanyika nchini Morocco.

    Akitaja kikosi kwenye mkutano wa waandishi wa Habari uliofanyika Makao Makuu ya TFF jijini Dar es Salaam, Kocha huyo alisema kambi hiyo ya matayarisho itakuwa Karatu mkoani Arusha.

    Alisema kambi hiyo itakuwa ya wiki tatu, na baadae kutafuta uwezekano wa kupata mechi za kirafiki.

    Wachezaji walioitwa ni Najiath Abbas (JKT Queens), Nusra Hamis (Fountain Gate Princess), Janeth Shija (Simba Queens), Enekia Kasonga (Gallos Femenil), Asha Omary (Simba Queens), na Ester Mabanza (Yanga Princess).

    Diana Mnaly (Yanga Princess), Donisia Minja (JKT Queens), Julietha Singano (FC Juarez), Noela Luhala (Mfazalgiris), Fatuma Issa (Simba Queens) na Anastazia Katunzi (JKT Queens), na Vaileth Nicholaus (Palm Hills SC).

    Ester Maseke (JKT Queens), Diana Lucas (Trabzonspor), Elizabeth Chenge (JKT Queens), Hasnath Ubamba (FC Masar), Stumai Abdallah (JKT Queens), Mary Siyame (Fountain Gate Princess), na Veronica Mapunda (Mashujaa Queens).

    Elizabeth Joseph (JKT Queens), Aliya Fikiri (JKT Queens), Bahati Steven (Bunda Queens), Opah Clement (EiBar), Rehema Ramadhani (Fountain Gate Princess), na Anastazia Shau (JKT Queens).

    Wengine ni Winfrida Charles (Fountain Gate Princess), Asha Mlangwa (JKT Queens), Clara Luvanga (Alnassr), Fatuma Aron (Yanga Princess), Winfrida Castor (JKT Queens) na Edna Makamba (Tausi FC).

    Twiga Stars ipo kundi ‘B’ na Afrika Kusini, Ivory Coast na Burkina Faso.

    Share.