Waamuzi wa FIFA, Elite wanolewa Dar

    Kozi ya waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), na wale wa ngazi ya Elite inaendelea jijini Dar es Salaam.

    Lengo la kozi hiyo inayofanyika kila robo mwaka ni kuwajengea uwezo wa kutafsiri na kutekeleza sheria za mpira wa miguu, na kupima utimamu wa mwili (fitness test).

    Kozi hiyo ya siku tano ilifunguliwa rasmi Julai 15 na Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani ambapo alisisitiza waamuzi kuzingatia sheria na kuzitafsiri kwa usahihi ili hadhi ya mpira wa miguu wa Tanzania izidi kupanda.

    Wakufunzi wa kozi hiyo ni Gladys Lengwe kutoka Zambia, na Mohamed Houssein Ali kutoka nchini Djibouti.

    Waamuzi 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika kozi hiyo itakayomalizika Julai 19, 2026.

    Waamuzi hao ni Ramadhan Kayoko, Henry Sassi, Ahmed Arajiga, Nasir Siyah, Tatu Malogo, Amina Kyando, Frank Komba, Kassim Mpanga, Ally Rajab, Jaman Ally, Mohamed Mkono, Janeth Balama, Glory Tesha na Zawadi Yusuph.

    Wengine ni Mary Selemani, Abdallah Mwinyimkuu, Alex Pangras, Sifu Msombwe, Haji Vemba, Anitha Kisoma, Yusuph Shombe, Black Tubuke, Mohamed Khamisi, Leonard Mkumbo, Ali Mbwana, Respicious Dismas, Shabani Musa, Edward Raphael, Juma Juma, Gladness Okeyo, Siraji Mkwaju na Mgisha Mikwalo.

    Share.