Twiga yaanza kwa ushindi WAFCON

    Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeanza vyema Fainali za WAFCON 2026 baada ya kupata ushindi kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini.

    Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Moulay Rachid jijini Casablanca tarehe 27 Julai ilimalizika kwa Twiga Stars kupata ushindi wa mabao 2-1.

    Mabao ya Twiga Stars yalifungwa na Diana Msewa dakika ya 36, huku dakika za jioni Hasnath Ubamba akitokea benchi akiiandikia timu yake bao la ushindi.

    Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime alisema bado timu yake ina kazi kubwa ya kufanya mbele ya Burkina Faso kwenye mechi inayofuata ili kujihakikishia kutinga hatua ya robo fainali.

    “Licha ya kupata ushindi huu, kwetu bado haijaisha tutarudi kufanya marekebisho uwanja wa mazoezi. Bado nilichotarajia kioneshwe na wachezaji kupitia mechi hii sijakipata ipasavyo,”alisema Shime.

    Twiga Stars inayoongoza kundi B itacheza mechi ya pili dhidi ya Burkina Faso tarehe 31 Julai.

    Share.