Tanzanite wanolewa kuhusu uadilifu

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeendesha warsha kuhusu uadilifu kwa kikosi cha timu ya Taifa (Tanzanite) kinachokwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 20.

    Warsha hiyo iliyobeba kaulimbiu ya “Hakuna Uvumilivu kwa Udanganyifu wa Matokeo ya Mechi,” Wachezaji na Viongozi wamepatiwa elimu kuhusu hatari na njia za kuripoti taarifa au matukio yoyote yenye kutilia shaka michezoni.

    Washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika 28 Agosti 2026 jijini Dar es Salaam walikumbushwa umuhimu wa kujiepusha na vitendo vya upangaji matokeo (match manipulation).

    Mwezeshaji katika Warsha hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Hassan Njama alitoa elimu kuhusu hatari zinazohusiana na upangaji wa matokeo.

    Wachezaji wakisisitiza dhamira yao ya kulinda uadilifu, usalama na ustawi wao, na kutovumilia vitendo vya udanganyifu, na kuzingatia misingi ya mchezo wa kiungwana (Fair Play).

    Mada nyinginge zilizojadiliwa kwenye Warsha hiyo ni Kutambua mbinu na njia zinazotumiwa kuwashawishi au kuwafikia wachezaji kwa lengo la kupanga matokeo ya mechi,
    Marufuku ya kushiriki katika kamari zinazohusiana na mashindano wanayoshiriki.

    Pia kutoa taarifa za ndani zinazoweza kutumiwa vibaya, Njia za siri za kuripoti matukio au majaribio ya upangaji wa matokeo, zinazopatikana saa 24 kwa siku, Madhara na hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya mtu anayehusika katika upangaji wa matokeo ya mechi.

    Share.