Nusu fainali mbili za Ngao ya Jamii kwa wanawake 2026 zitachezwa tarehe 30 Septemba katika Uwanja wa KMC uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

    Ngao ya Jamii ambayo ni ishara ya kufunguliwa kwa pazia la Mashindano ya Wanawake msimu wa 2026/2027 itazikutanisha timu za JKT Queens na Mashujaa, mechi itakayoanza saa 9 kamili alasiri.

    Nusu Fainali ya pili ambayo itawakutanisha mabingwa watetezi Simba Queens dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Princess itachezwa kuanzia saa 12 kamili jioni.

    Timu zitakazoshinda mechi za nusu fainali zitacheza fainali wakati zilizoshindwa zitacheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu. Mechi za fainali na mshindi wa tatu zitafanyika tarehe 3 Oktoba.

    Katika hatua nyingine, Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL) itaanza tarehe 23 Oktoba 23,2026.

    Share.