Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanaume U20 (Ngorongoro Heroes), Mario Rivera amesema kutokana na umuhimu wa mchezo wa kesho dhidi ya Burundi kwao ni sawa na fainali.

    Mario amesema wakishinda mchezo huo utaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mbali na kucheza fainali ya michuano hiyo watakuwa wamefuzu AFCON 2027.

    Amesema anajua ubora wa wapinzani wao lakini wamejiandaa vizuri na wachezaji wameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwasapoti vijana wake.

    Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Arafat Ally amesema benchi la ufundi limemaliza kuwafundisha mbinu za kuibuka na ushindi kilichobaki ni wao kwenda kutelekeza uwanjani na wanaamini watafanya vizuri.

    Ngorongoro Heroes imefanikiwa kutinga katika hatua hiyo baada ya kuichapa Rwanda kwa mabao 3-0 kabla ya kuitandika Ethiopia kwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

    Share.