Timu ya Taifa ya Tanzania ya FUTSAL itaanza kampeni ya kuwania taji la AFCON 2026 dhidi ya Misri Okoba 13, 2026.

    Katika michuano hiyo, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Oktoba 12 mpaka 21 mwaka huu, Tanzania imepangwa kundi B pamoja na Misri, Angola na Msumbiji.

    Baada ya mchezo dhidi ya Misri, itashuka tena uwanjani Oktoba 15 dhidi ya Angola, kabla ya kumalizana na Msumbiji Oktoba 17.

    Michuano hiyo itafanyika nchini Morocco.

    Share.